Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, maandamano haya makubwa ni mkusanyiko wa tatu wa wananchi tangu kurejea kwa Trump Ikulu ya White House. Miongoni mwa sababu zilizopelekea kufanyika kwa maandamano haya ni kufungwa shughuli za serikali kuu, jambo lililosababisha kusitishwa kwa huduma na programu za serikali ya shirikisho. Wataalamu wanaona hali hii kuwa ni jaribio la Trump kupima mizani ya nguvu za nyuklia na mamlaka binafsi katika mchezo huu wa kisiasa, huku ikionekana wazi kuwa sasa taasisi ya utendaji (serikali kuu) nchini Marekani imeanza kuonesha mienendo ya kichokozi dhidi ya Bunge na Mahakama. Hali hii, kwa mujibu wa wachambuzi, ni hatua hatari inayorudisha taifa hilo katika mfumo wa kiimla na udikteta wa utawala.
Waandaaji wa tukio hili kubwa wamesisitiza kuwa mikusanyiko hiyo imefanyika katika zaidi ya matukio 2,600 nchini Marekani.
Inapaswa kusemwa pia kuwa maandamano haya yalianza nje ya Marekani, yakianzia mbele ya Ubalozi wa Marekani mjini London, ambapo mamia ya waandamanaji walikusanyika, kisha wakiungwa mkono na mamia wengine katika miji ya Madrid na Barcelona. Baadaye, kaulimbiu hii ya “Hapana Ufalme!” ikawa wimbo mkuu wa maandamano ya wananchi kote Marekani.
Chanzo: Al Jazeera
Maoni yako